Wednesday, 24 August 2016

WHERE YOU ARE ???

WATU SABA MUHIMU (SEVEN IMPORTANT PEOPLE B4 THE GOD)
Kuna maandiko tofauti yaliokuja na kuweka wazi watu walibora na muhimu mbele ya mola wao. Takriban mifumo yote imeonesha watu hao kulingana vitabu vyao vinavyoonyesha. Moja ya maandiko imeonesha watu saba muhimu mbele ya mola wao na hii kutokana na tabia na mwenendo wa watu hao. 
1. Kiongozi Mwaadilifu
2. Kijana aliyekulia katika kumwabudu mola wake.
3. Mtu ambaye moyo wake umefungamana katika nyumba ya ibada
4. Watu wawili waliopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu
5. Mwanaume aliyeombwa zinaa na mwanamke mwenye hadhi na uzuri akaseme; mimi namuogopa Mwenyezi Mungu.
6. Mtu aliyetoa sadaka akaificha watu wasijue ametoa nini.
7. Mtu aliyemkumbuka mola wake akiwa faragha mpaka akali.

Be among those seven people!

FROM:
TAILORING DESIGNER
WAUZAJI NA WASHONAJI WA SARE ZA SKULI (UNIFORMS)
FUONI MAHARIBIKO - ZANZIBAR
0718001830 

SARE ZA SHULE 2016/2017

KWA NINI USUMBUKE MSIMU HUU WA MASOMO 2016/2017 ?

TAILORING DESIGNER
Msimu huu wa masomo 2016/2017 tunatarajia kushona na kuuza
sare za skuli (uniforms) zaidi ya skuli 30 zinazopatika Unguja.
Sare zitakazo patikana ni :-
Sare za Skuli za Serikali, Glorious, Laurent, High Performance,
Mbarali, Hill Hop, Alharamain, Trifonia, Hifadhi na
Skuli zote wanazovaa shirt nyeupe na suruali nyeusi.
TAILORING DESIGNER UNIFORM DEALER
Access to Shine
FUONI – MAHARIBIKO
ZANZIBAR
Add caption

WASIYA WA BABA KWA MTOTO WAKE


1. Mwanangu ninaposema wewe utakuwa kichwa cha nyumba katika ndoa yako, simaanishi uwezo wako wa kipesa na kutunza familia. Bali ni kuhakikisha kila siku tabasamu la mkeo halitoweki.


2. Mwanangu kumbuka, pale utakaposema mke wangu amebadilika, basi ujue kuna kitu wewe umesitisha kumfanyia.
3. Mwanangu mama yako aliendesha baiskeli na mimi kabla sijapata visenti vya kununulia motokaa. Mwanamke yeyote ambae hatakuwa na weww wakati wa shida kamwe asifurahie matunda uliyovuna.

4. Mwanangu, usimfananishe mkeo na wanawake wengine, kuna mambo ambayo na yeye anakuvumilia tu! Kwani ashawahi kukufananisha na wanaume wengine?

5. Mwanangu, usijisahau pale utakapofanikiwa kutengeneza pesa, badala ya kutumia hizo pesa na wanawake vicheche ambao hawajui ni jinsi gani ulivyozihangaikia, ni bora ukatumia na mwanamke ambae alisimama bega kwa bega na wewe mpaka ukawa nazo

6. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa sababu nilikuwa mpumbavu kwa kufikiri kusomesha watoto wa kike ni hasara. Tafadhali sana nawe usifanye kosa hilo. Mafanikio nayoyaona hivi sasa kwa wanawake yamewafanya wawe wa muhimu sana. Wasomeshe watoto wote kwa usawa.

7. Mwanangu, mimi na mama yako hatuko interested na kike kitakachokua kikitokea katika ndoa yenu, jaribuni kusuruhisha mambo yenu wenyewe pasina kuja kwetu.

8. Mwanangu, kumbuka nilimnunulia mama yako cherehani yake ya kwanza. Msaidie mkeo azifikie ndoto zake kama jinsi wewe unavyojitahidi kufikia malengo yako.

La muhimu mwanangu, Omba Mungu na familia yako, kuna kesho ambayo hauijui. Ongea na Mungu kwa sala kwani yeye ndiye ajuaye kesho zetu....
Nakupenda Mwanangu, nenda ukawe Mume Bora, kamwe usiniangushe.

TAILORING DESIGNER
TUNAUZA NA TUNASHONA SARE ZA SHULE AINA ZOTE.
FUONI - ZANZIBAR.
0718001830
Tailoring Designer - Access to Shine !!!
We offer you the best because you deserve it.
 

VIPI NITAKUA MJASIRIAMALI (ENTREPRENEUR) !

FUNZO KWA WAJASIRIAMALI
Kama unachipukia au ndo unaendelea katika ujasiriamali (biashara), jaribu kufuata na kuzingatia mambo yafuatayo :- 
1. Start with small; Think Big (Anza na kidogo; fikiria cha juu zaidi). Nafikiria kama unataka kuwa mjasiriamali (mfanya biashara) mwenye mafanikio na huna uwezo wa kugharamia namna ya kuwa namna hio, unahitajika uamini kwamba unaouwezo wa kubadili mazingira yako kwa kile kitu unachokifanya....

2. Money will follow (Pesa itakutafuta na kukufata). Unapoanzisha ujasiriamali au biashara yoyote uzianzishe kwa sababu ya kupata pesa pekee, ni lazima uanzishe kutokana na ujuzi na hamu (Passion) ulionayo juu ya biashara hio badala ya Pesa. Ni muhimu sana kutambua punde biashara yako itakapo kua (grow) upatikanaji wa pesa hautoepukika.
 
3. Enjoy it (Furahia kile unachokifanya). Jaribu kuvutiwa na kukipenda kile ulicho kianzisha, kwasababu isipokipenda kuna uwezekano wa kupata tabu kukiendesha kwa muda mrefu (will be suffering a very long time)

4. Hard work and determination (Fanya kazi kwa bidii na Hamasa). Kwa ushirikiano na wenzio (team) unakupasa ufanye kazi kwa bidii hususani katika kutafuta utatuzi (solution) wa matatizo katika biashara husika.
WILL CONTINUE !!!
 
 TAILORING DESIGNER - UNIFORM DEALER
FUONI - MAHARIBIKO
ZANZIBAR.
0718001830. 
ULIPO TUPO; UNGUJA - ZANZIBAR